Mara kwa mara kumekua na usumbufu mwingi kuhusiana na "last seen", last seen imesababisha matukio mengi hasa kwa watu walio kwenye uhusiano. Mara nyingi mtu huona ni muda gani rafiki yake/mchumba wake ameacha kuonekana online, hivyo wakati mwingine kuleta mzozo.
Kuna njia mbili za kufanya ili kutoa last seen kwenye whatsapp.
Kuna njia mbili za kufanya ili kutoa last seen kwenye whatsapp.
Kwa kutumia application (kwa watumiaji wa Android SmartPhone)
Kuna application inaitwa last not seen hii huzui WhatsApp kuupdate status yako. Application hii haipo bado kwenye store ya google (play store) hivyo itakulazimu utafute package yake na udownload package yake (apk) kwa kuitafuta kwenye google.
Inafanyaje kazi?
Hii huzuia internet connection mara tu unapolaunch application ya WhatsApp, hivyo servers za WhatsApp haziwezi kuupdate muda ambao umesoma meseji ya mwisho.
1. Download na uiinstall hiyo application https://app.box.com/s/lxf9m0eq6m7pc4drvdqb .
(Nimekusaidia link yake hapo)
(Nimekusaidia link yake hapo)
2. Fungua application yako utaona vibox vitatu tick box lililoandikwa block last seen .
Sasa fungua application yako ya WhatsApp, utagundua kua internet yako imekata automatically, mara tu utakapotoka WhatsApp huduma ya internet itarudi kama kawaida.
Bila kutumia application (Manually disable Last Seen on WhatsApp)
1. Zima internet connection yako.
2. Fungua application yako ya WhatsApp, soma meseji zote na utume meseji unazotaka kutuma.
3. Funga application yako na washa internet yako. Mara tu utakaporuhusu internet connection Whatsapp itasync na servers na itatuma message zote ulizoziandika bila server kutambua ni wakati gani umesoma na kutuma meseji hizo.
Kwa watumiaji wa iPhone
Ni rahisi sana kwa watumiaji wa iPhone kutoa last seen
nenda settings>>Advanced>>Last seen Timestamp na uizime hiyo timestamp
Kwa watumiaji wa blackberry,windows phone na Symbian phones wanaweza fanya hivyo kwa kutumia manual disable last seen kama nilivyoelezea hapo juu.
By Nteminyanda Godfrey S.
UNIVERSITE MENTOURI DE CONSTANTINE - CONSTANTINE, ALGERIA.
OMBI: Acha comment kama nimekusaidia katika tatizo hili







